

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atia saini amri juu ya kutunuku utafiti wa kisayansi wa mambo ya kijeshi
BEIJING – Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametia saini amri ya kutolewa kwa kanuni juu ya kutunuku utafiti wa kisayansi wa mambo ya kijeshi.
Waraka huo mpya ambao utafanya kazi kuanzia Julai 1, unalenga kutekeleza mkakati wa kuimarisha majeshi kwa njia ya sayansi na teknolojia na kukamilika kwa utaratibu wa utoaji tuzo za utafiti wa kisayansi wa mambo ya kijeshi.
Kanuni hizo zinaanzisha mfumo wa kutunuku uliopangiliwa vema kulingana na malengo ya mikakati ya nchi na ya mambo ya kijeshi na umaalumu muhimu wa kanuni hizo ni kuamua uwezo na nguvu ya mapambano kuwa kigezo pekee cha tuzo, kukamilisha taratibu za uteuzi na ukaguzi wa tuzo, na kuimarisha usimamizi juu ya nidhamu na uhifadhi wa siri.
Kanuni hizo zinatarajiwa kuimarisha hamasa ya uvumbuzi katika utafiti wa mambo ya kijeshi, kuharakisha mafanikio mapya katika teknolojia ya ulinzi wa nchi, na kutoa uungaji mkono wa kisayansi wa hali ya juu kwa ajili ya mambo ya kujenga jeshi lenye nguvu katika zama mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma