Msemaji: Oda kutoka kwa Marekani zaongezeka baada ya mkutano wa China na Marekani huko Geneva

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2025

BEIJING - Baada ya mkutano wa uchumi na biashara mjini Geneva mapema mwezi huu kupunguza mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani, oda kutoka kwa wanunuzi wa Marekani zimeongezeka maradufu, na huduma za usafirishaji wa meli zimekuwa zikifanya kazi katika uwezo kamilifu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema.

"Hii inaonyesha vya kutosha mahitaji makubwa kutoka kwa kila moja ya nchi hizo mbili," msemaji Mao amesema katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano.

Maneno hayo yanatokana na maoni ya mkuu wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani nchini China Michael Hart kwenye Mkutano wa Kilele wa Kuhimiza Biashara na Uwekezaji Duniani 2025 mjini Beijing wiki iliyopita. Hart alisema China ni soko muhimu la jumla na muuzaji wa bidhaa kwa Marekani.

“Msingi wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni wa kunufaishana kwa pande zote” msemaji huyo amesema, akiongeza kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani umeleta manufaa halisi kwa viwanda na watumiaji wa nchi hizo mbili.

Akisema kuwa kujilinda kibiashara kunashindwa kuelekea popote, China inakaribisha viwanda vya kote duniani pamoja na viwanda vya Marekani kuja China kuanzisha shughuli zao na kujiendeleza, kuzidisha ushirikiano na China, na kunufaika pamoja na fursa zinazotokana na ushirikiano huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha