

Lugha Nyingine
Mameya kutoka nchi mbalimbali duniani wakusanyika Shanghai kwa mazungumzo ya ushirikiano
Wageni wakihudhuria mkutano wa Mazungumzo ya Mameya Duniani na Baraza la Kimataifa la Ushirikiano wa Miji ya Urafiki la Shanghai 2025 mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 29, 2025. (Xinhua/Wang Xiang)
SHANGHAI - Mameya na wawakilishi wa miji 26 kutoka nchi 22 wanakusanyika mjini Shanghai, mashariki mwa China kuhudhuria mkutano wa Mazungumzo ya Mameya Duniani na Baraza la Kimataifa la Ushirikiano wa Miji ya Urafiki la Shanghai 2025, ambao umeanza Jumatano wiki hii.
Mabadara madogo ya mkutano huo yana kaulimbiu ya "Uwezeshaji wa nishati kijani na utoaji wa kaboni chache kwa maendeleo endelevu mijini" na "Kuhamasisha uhai wa vijana kwa uvumbuzi wa mji katika siku za baadaye." Baraza hilo litaendelea hadi kesho Jumamosi.
“Huku ikiendeleza uhusiano wa miji-dada chini ya hali ngumu na inayobadilika sana ya kimataifa, miji hiyo inahitaji kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, kuimarisha urafiki wa muda mrefu wenye msingi wa usawa, kuaminiana na kushauriana kwa pamoja, na kunufaishwa na fursa za maendeleo kwa pamoja, yote hayo yakiwa na lengo la kuhimiza ustawi na utulivu,” Meya wa Shanghai Gong Zheng amesema kwenye mkutano huo.
Haris Doukas, meya wa Athens, Ugiriki, amesisitiza umuhimu wa diplomasia ya mji katika kukabiliana na janga la tabianchi.
"Diplomasia ya mji imewezesha miji kuongoza njia, kufikia ushirikiano muhimu wa kuzuia, kunufaishwa na ujuzi, kuweka malengo jasiri na halisi kupitia ushiriki katika mitandao na mabaraza ya kimataifa, na kupunguza mizigo yanayotokana na janga la tabianchi," Doukas amesema.
Shanghai na Athens zilianzisha uhusiano wa miji-dada mwezi Januari mwaka huu.
"Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kuu inayokabili dunia yetu ya leo," amesema Dan Boyle, meya mkuu wa Cork, Ireland, akiongeza kuwa "moyo wa ushirikiano wa kimataifa, ambao unaonyeshwa kwenye mikutano kama ya leo, unaweza kutupa matumaini kwamba changamoto hii inayokabili binadamu wote itatimizwa."
Dan Boyle meya wa Mji wa Cork wa Ireland akizungumza kwenye mkutano wa Mazungumzo ya Mameya Duniani na Baraza la Kimataifa la Ushirikiano wa Miji ya Urafiki la Shanghai 2025 mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 29, 2025. (Xinhua/Wang Xiang)
Haris Doukas meya wa Mji wa Athens, Ugiriki akizungumza kwenye mkutano wa Mazungumzo ya Mameya Duniani na Baraza la Kimataifa la Ushirikiano wa Miji ya Urafiki la Shanghai 2025 mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 29, 2025. (Xinhua/Wang Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma