

Lugha Nyingine
Uganda yaanzisha hojaji kukusanya taarifa za VVU ili kutathmini upigaji hatua na kuongoza hatuza za siku zijazo
Wizara ya Afya ya Uganda imeanzisha hojaji ya kukusanya taarifa za VVU kote nchini humo kupitia duru ya tatu ya Tathmini ya Athari za VVU kwa Watu wa Uganda (UPHIA) 2025, ili kutathmini upigaji hatua uliofikiwa katika kupambana na virusi hivyo na kutoa mwongozo kwa hatua za siku zijazo.
Akitangaza rasmi kuanza kwa duru hiyo, Waziri wa Afya wa Uganda, Ruth Aceng amesema hojaji hiyo ya kukusanya taarifa inalenga kutathmini ufanisi wa programu za sasa za VVU nchini humo, kutafuta mianya, na kutoa taarifa juu ya mikakati itakayotolewa.
Ikifanywa kwa ushirikiano na Ndaki ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Makerere na Idara ya Takwimu ya Uganda, hojaji hiyo ya kukusanya taarifa ambayo ni ya washiriki wa hiari na watakaopatikana kwa njia ya kuteuliwa bila mpangilio maalum itahusisha washiriki takriban elfu 15 wenye umri wa miaka 15 na zaidi, waliochaguliwa kutoka kaya 6,685 kote nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma