Ujumbe wa UN watoa wito wa kuwepo kwa amani ya kudumu nchini Sudan Kusini

(CRI Online) Mei 30, 2025

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa jana Alhamisi ukitoa wito wa amani ya kudumu nchini humo.

Hafla hiyo iliyofanyika Juba, ilishuhudia washiriki wakitambua ujasiri na kujitolea kwa walinda amani 18,000 waliovalia sare na waliovalia kiraia ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatari kuiunga mkono Sudan Kusini.

Naibu mwakilishi maalum kwa Sudan Kusini ambaye pia ni naibu mkuu wa UNMISS Guang Cong amesema jukumu la ujumbe huo ni kuunga mkono pande zote zinazoongoza mabadiliko ya Sudan Kusini.

“Sisi, pamoja na washirika wetu wa kikanda na kimataifa, tunahimiza pande husika katika makubaliano ya amani kutatua mivutano kupitia mazungumzo, kujenga imani na kujiamini, kuhakikisha usitishaji uhasama, na kuchukua hatua hitajika kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani.” Amebainisha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha