

Lugha Nyingine
Tanzania yashuhudia kuongezeka kwa utalii wa matibabu kufuatia uwekezaji mkubwa katika huduma za afya
Waziri wa Afya wa Tanzania Jenista Mhagama amesema nchi hiyo inashuhudia ukuaji mkubwa wa utalii wa matibabu ambao unahimizwa na uwekezaji mkubwa wa serikali katika huduma za afya.
Akizungumza katika kikao cha Bunge la Tanzania katika Mji Mkuu wa Dodoma, Bi. Mhagama amesema kati ya mwaka 2021 na mwezi Machi mwaka 2025, idadi ya wagonjwa wa kimataifa iliongezeka kutoka 5,705 hadi 12,180, na kwamba wagonjwa hao wanatoka nchi mbalimbali zikiwemo Visiwa vya Comoro, Malawi, Burundi, Zambia, Rwanda, Afrika Kusini, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Uganda, Zimbabwe, Ethiopia, Somalia, Kenya, Misri na Mauritius.
Pia amesema ongezeko hilo limeonesha ongezeko la ushawishi wa Tanzania kwenye sekta ya afya katika kanda hiyo, haswa katika nyanja za saratani, magonjwa ya moyo na mifupa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma