Raia 105 wa Rwanda waokolewa kutoka biashara haramu ya binadamu

(CRI Online) Juni 03, 2025

Raia 105 wa Rwanda wameokolewa kutoka biashara haramu ya usafirishaji binadamu tangu mwezi Juni mwaka jana hadi mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali, msemaji wa Mamlaka ya Upelelezi ya Rwanda Thierry Murangira amesema, wengi wa waathirika waliuzwa katika nchi mbalimbali, huku 57 wakiokolewa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

Amesema wafanya biashara hiyo haramu ya usafirishaji binadamu wanashirikiana na mawakala wakitumia mtandao kuvutia waathirika kwa kuwapa ahadi za uongo za kazi nzuri na ufadhili wa masomo.

Mwezi Mei, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alisema, watu 10 wameokolewa kutoka Myanmar na kurejeshwa nchini humo kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha