Mji wa Beijing, China waboresha huduma za usafiri wa kuingia huku wageni wakiongezeka Januari-Aprili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2025
Mji wa Beijing, China waboresha huduma za usafiri wa kuingia huku wageni wakiongezeka Januari-Aprili
Mtalii wa kigeni akinunua kofia kwenye duka la kofia la Shengxifu la Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 22, 2025. (Xinhua/Li Xin)

BEIJING – Mji Mkuu wa China, Beijing umezindua mpango wa utekelezaji wa jumla wa kuboresha huduma zake za utalii kwa wageni watalii jana Jumanne katika Mkutano wa Maendeleo ya Utalii wa Wageni Wanaotembelea Beijing, huku mji huo ukiripoti ongezeko la asilimia 57.1 la watalii wageni wa ng'ambo wakifikia milioni 1.46 kutoka Januari hadi Aprili.

Mpango huo unawekwa hatua 22 zinazohusu bidhaa, ukuzaji, huduma na uungaji mkono -- ukilenga kuongeza mvuto wa mji wa Beijing, ambapo unaeleza kuwa juhudi kuu za bidhaa zinahusu kunadi chapa ya " Mstari wa Katikati ya Beijing " na kuwa na huduma za shughuli mbalimbali za utalii katika pande mbili za “Mstari wa Katikati ya Beijing” kama vile kutembelea sehemu za mali ya urithi wa dunia, kutembelea kwenye vichochoro yaani Hutong za Beijing, na kuendesha baiskeli kwenye njia ya pande mbili za mstari wa katikati ya Beijing.

Aidha mpango huo unaweka mkazo katika huduma katika kupanua na kuboresha mitandao ya kimataifa ya ndege, kurahisisha utaratibu wa kuingia kwa maeneo maalum ya "vibali vya muda vya kuingia" kwa utoaji huduma zote katika kituo kimoja, na kuwezesha kadi nyingi za benki za kigeni kwa matumizi ya malipo ya usafiri wa njia sabwei ili kuinua urahisi.

"Shughuli za utalii wa wageni kutoka nje wanaotembelea Beijing zinaendelea kustawi vizuri, idadi ya watalii wageni inaongezeka siku hadi siku na matumizi pia yamefikia ya juu," amesema Sima Hong, naibu meya wa Beijing, akiongeza kuwa mji wa Beijing una shauku ya kushirikiana na washirika wa kimataifa ili kuwasha wimbi la “Kutalii Beijing ", na kuwapa watalii hali ya uwazi, rahisi na ya kuvutia zaidi.

Kwenye mkutano huo, njia 10 mpya za vivutio maalumu zimeanzishwa chini ya bendera ya "Uvumbuzi Mpya wa Beijing", ikihusisha safari za kutafuta vyakula vitamu, kujaribu na kujionea mali ya urithi wa utamaduni usioshikika na utalii wa mandhari wa usiku kwa kutumia boti, ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya watalii.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha