

Lugha Nyingine
Wang Yi akutana na Balozi wa Marekani nchini China, akitumai atahimiza uhusiano kati ya nchi mbili kuendelezwa vizuri, kithabiti na endelevu
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Balozi mpya wa Marekani nchini China David Perdue mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 3, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amemkaribisha Balozi mpya wa Marekani nchini China David Perdue jana Jumanne na kueleza matumaini yake kuwa atachukua jukumu kubwa katika kuhimiza maendeleo mazuri, thabiti na endelevu ya uhusiano kati ya pande mbili.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa kauli hiyo alipokutana na Perdue mjini Beijing, akieleza matumaini kwamba Perdue atafanya kazi kama mwasilishaji wa kutegemewa, mpatanishi juu ya tofauti na mhimizaji wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
“Uhusiano kati ya China na Marekani kwa sasa uko katika wakati muhimu na wa kimabadiliko,” Wang amesema, akieleza kuwa, kwa kutazama nyuma katika safari ya takriban miaka 50 iliyojaa misukosuko na mageuzi tangu kuanzishwa kwa uhusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ufunuo muhimu zaidi ni kwamba usawa na heshima ni masharti ya mawasiliano kati ya pande hizo mbili, na kwamba mazungumzo na ushirikiano ndiyo chaguo pekee sahihi.
Wang amesisitiza kuwa baada ya mazungumzo ya uchumi na biashara ya pande mbili mjini Geneva, China imetekeleza kwa makin maafikiano yaliyofikiwa na pande zote mbili.
"Lakini, inasikitisha kwamba Marekani tangu wakati huo imeanzisha hatua hasi mbalimbali zisizo na msingi, ikikiuka haki na maslahi halali ya China. China inapinga vikali vitendo hivyo," amebainisha.
Wang amesema upande wa Marekani unapaswa kuendana na China, kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa mazungumzo yao ya simu Januari mwaka huu, na kuweka mazingira muhimu ya kurejesha uhusiano wa pande mbili kwenye njia sahihi.
Kwa upande wake Perdue amesema Rais Donald Trump anamheshimu sana Rais Xi Jinping, akisema kuwa ni muhimu sana kwa wakuu hao wawili kuendelea na mazungumzo chanya na ya kiujenzi.
Perdue pia amesema, akiwa balozi wa Marekani nchini China, angependa kufanya mawasiliano ya karibu na China katika moyo wa kuheshimiana na mazungumzo makini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Balozi mpya wa Marekani nchini China David Perdue mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 3, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma