Lee Jae-myung aapishwa rasmi kuwa Rais wa Korea Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2025

Lee Jae-myung na mkewe Kim Hye-kyung wakishangilia kwenye Bunge la Taifa mjini Seoul, Korea Kusini, Juni 4, 2025. (Xinhua/Yao Qilin)

Lee Jae-myung na mkewe Kim Hye-kyung wakishangilia kwenye Bunge la Taifa mjini Seoul, Korea Kusini, Juni 4, 2025. (Xinhua/Yao Qilin)

SEOUL –SEOUL - Lee Jae-myung ameapishwa kuwa rais mpya wa Korea baada ya kuanza rasmi muhula wake wa kwanza wa miaka mitano mapema leo Jumatano ambapo rais huyo wa 21 wa nchi hiyo amekula kiapo katika jengo la Bunge la Taifa, akisema katika hotuba yake ya uapisho kwa njia ya televisheni kwamba atatumikia watu wote waliyemuunga mkono katika uchaguzi huo wa rais.

Lee Jae-myung ambaye ni wa Chama cha Kidemokrasia cha kiliberali chenye wabunge wengi amepata asilimia 49.42 ya uungwaji mkono, akimshinda mpinzani wake mkuu Kim Moon-soo wa chama cha kihafidhina cha People Power kwa tofauti kubwa ya asilimia 8.27.

Shirika la utangazaji nchini humo JTBC na mashirika mengine matatu ya utangazaji ya nchi hiyo, yakiwemo KBS, MBC na SBS yalikuwa yametabiri mapema kwamba Lee alikuwa na uhakika wa kuchaguliwa kuwa rais wa 21 wa nchi hiyo.

Idadi ya awali ya wapigakura waliojitokeza ilifikia asilimia 79.4, ikimaanisha idadi kubwa zaidi ya wapigakura katika kipindi cha miaka 28 tangu kiwango cha wapigakura kiliporekodi asilimia 80.7 mwaka 1997.

Miongoni mwa wapiga kura wapatao milioni 44.39 waliotimiza vigezo vya kupiga kura, watu milioni 35.24 wamepiga kura zao katika vituo 14,295 kote nchini humo.

Idadi ya wapiga kura waliojitokeza, ambayo inajumuisha wale walioshiriki katika upigaji kura wa mapema Alhamisi na Ijumaa wiki iliyopita, imeongezeka kutoka asilimia 77.1 iliyorekodiwa katika uchaguzi uliopita wa urais mwaka 2022.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha