

Lugha Nyingine
Wabunge Tanzania walalamikia gharama za vifurushi vya matibabu
Mjadala mkali umeibuliwa na wabunge wakati Bunge la Tanzania likipitisha bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/26, ambapo wabunge walikuwa wakihoji gharama za vifurushi vya bima ya afya na matibabu ya ugonjwa wa figo.
Akizungumza bungeni jana Jumanne, mbunge mmoja wa viti Maalumu, amesema kwa mujibu wa kitabu kilichotolewa na Wizara ya Afya, utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza ulifanyika mwaka 1987, na kwamba mkazo kwenye baadhi ya magonjwa hauendani na hali halisi ya vifurushi vya matibabu.
Ametolea mfano wa ugonjwa wa kisukari ambao mwaka 1987 ulimwathiri mtu mmoja kati ya 100, lakini utafiti wa mwaka 2012 unaonesha kuwa ugonjwa huo ulikuwa ukiathiri watu 26 kati ya 100.
Ameihimiza na kuishauri serikali kuwekeza zaidi kwenye magonjwa hayo na hata kuhimiza uwepo wa programu za mazoezi, ikiwa ni pamoja na kuangalia jinsi ya kuweka njia na sehemu za kukimbia mitaani, ili watu wakitoka kazini wapate maeneo ya kufanyia mazoezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma