Uzuri wa Majira: Nafaka katika masuke

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2025

Habari zenu! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Kesho alhamisi itakuwa Mangzhong, au kipindi cha “Nafaka katika Masuke” katika vipindi 24 vya hali ya hewa katika kalenda ya jadi ya China, kinachomaanisha mwanzo wa katikati ya majira ya joto. Ungana nami kutembelea kijiji kizuri cha Hongcun mkoani Anhui, mashariki mwa China, ili kugundua mvuto wa kipindi hiki katika kalenda ya jadi ya China.

“Kama mbegu hazijapandwa hadi kufikia kipindi cha Mangzhong, ni bure kuzipanda kabisa.” Methali hii inaonesha ufahamu sahihi wa wakulima wa kale wa China wa nyakati za kilimo. Katika kipindi hiki, watu wa kusini mwa China hupanda mpunga huku wa kaskazini wakivuna ngano. Watu hufanya kazi kwa bidii mashambani, wakijenga taswira ya pilika nyingi.

Wakati wa kipindi hiki cha Mangzhong, Delta ya Mto Yangtze huingia "msimu wa mvua za plamu", jina linalotokana na msimu wa kukomaa kwa matunda ya plamu. Katika kijiji cha Hongcun, manyunyu ya mvua huunda hali ya ukungu kama hadhiti ya kichimbakazi. Kuta nyeupe na vigae vyeusi vya majengo yenye usanifu wa Huizhou kwa uzuri huungana na vilima vya kijani na mito, vikiunda mandhari inayofanana na mchoro wa wino wa kijadi wa China.

Kipindi cha Mangzhong kinapofika, msimu wa kuchanua kwa maua huelekea mwisho. Watu hufanya shughuli za kumuaga mungu wa maua ili kuonesha shukrani na kutakia ustawi wa maua kwa mwaka ujao. Maeneo mengi duniani pia huheshimu maua. “Tamasha la Waridi” la kila mwaka nchini Bulgaria huhusisha kuimba na kucheza ili kusherehekea mavuno ya waridi. Upendo huu wa pamoja kwa uzuri wa mazingira asili huvuka mipaka.

“Angalia tu tambarare ya ukungu ambako majani huota kuwa msitu, mivinje ikipepeshwa na upepo, au manyunyu ya mvua yakigeuza miti ya plamu kuwa ya njano!” Katika msimu huu wa juhudi za bidii na ahadi ya mavuno, ni mbegu gani za matumaini na ndoto ungependa kupanda?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha