Xi Jinping akutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing, China, Juni 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing, China, Juni 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing jana Jumatano, ambapo alimpongeza Lukasjenko kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Belarus, na kusema kuwa nchi hizo mbili ni marafiki wa kweli na washirika wazuri, zikitendeana kwa udhati na kuaminiana.

Rais Xi amesema kuwa China na Belarus zinashikilia kithabiti urafiki wa kudumu wa jadi, kuaminiana kisiasa bila kujali chochote, na ushirikiano kati yao unaendelea kwa pande zote katika sekta mbalimbali, na China daima inatendea na kuendeleza uhusiano kati ya China na Belarus kutoka mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu.

Rais Xi amesema China inapenda kujiunga na Belarus katika kuhimiza maendeleo ya kithabiti ya uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Ametoa wito kwa pande zote mbili kuimarisha zaidi uratibu na ushirikiano ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, kwa pamoja kupinga umwamba na uonevu, na kulinda haki na usawa wa kimataifa.

Kwa upande wake Rais Lukashenko, ambaye yuko katika ziara yake ya 15 nchini China, amesema kwamba amehisi hisia ya urafiki wa kweli kutoka China wakati wa kila ziara yake.

Akiishukuru China kwa uungaji mkono na msaada wake wa muda mrefu kwa nchi yake, amesema Belarus ina imani ya juu kwa China na itafanya juhudi za kuhimiza ushirikiano na China.

Rais Lukashenko amesema China imeweka mfano wa kuigwa kwa dunia kwa kushikilia ushirikiano wa pande nyingi na kupinga maamuzi ya upande mmoja na vikwazo na shinikizo, upande wa Belarus inasifu sana China, na inapenda kufanya juhudi na China ili kulinda pamoja haki na usawa wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha