Rais Xi ampongeza Lee Jae-myung kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Korea Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano ametoa pongezi kwa Lee Jae-myung kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Korea Kusini, akisema kuwa China na Korea Kusini, kila moja ni majirani muhimu wa karibu na mshirika wa ushirikiano kwa nchi nyingine kati yao.

Rais Xi amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 33 iliyopita, pande hizo mbili zimevuka tofauti za itikadi na mfumo wa jamii, kusonga mbele bega kwa bega na kupata maendeleo kwa pamoja, na kuufanya uhusiano kati yao uendelee vizuri kwa utulivu.

"Hii si tu imeboresha ustawi wa watu wa nchi hizo mbili, bali pia imetoa mchango wa kuongeza hamasa kwa ajili ya kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda," Rais Xi ameongeza.

Rais huyo wa China amesisitiza kutilia maanani zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na Korea Kusini.

"Katika dunia leo, mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita yanatokea kwa kasi kubwa zaidi, na mambo ya kuvuruga utulivu katika hali ya kimataifa na kikanda yanaongezeka," Rais Xi amesema.

Amesema nchi mbili zikiwa nchi muhimu duniani na katika kanda, China inapenda kushirikiana na Korea Kusini katika kuendelea kufuata kithabiti nia ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia, kushikilia mwelekeo wa ujirani mwema na urafiki , na kushikilia lengo la kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, na kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya siku hadi siku ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Korea Kusini, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha