China yasisitiza kuwa suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China na halipaswi kulinganishwa na mgogoro wa Ukraine

(CRI Online) Juni 05, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesisitiza kuwa, Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya China, na kwamba suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China, na halipaswi kulinganishwa na mgogoro wa Ukraine.

Lin ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano, ambapo pia amesema China inapinga vikali kauli na vitendo vyovyote vinavyojaribu kuchanganya au kupotosha ukweli kuhusu suala la Taiwan.

Amehimiza pande husika kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja kwa vitendo halisi, na kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China.

Hayo yamekuja baada ya kiongozi wa Ulaya aliyeshiriki mkutano wa hivi karibuni wa Mazungumzo ya Shangri-La nchini Singapore kulinganisha suala la Taiwan na mgogoro huo wa Ukraine, akitoa kisingizio cha "tishio la China" kwa kutumia suala la Bahari ya Kusini, huku akisema NATO "ina sababu ya kuingilia kati katika eneo la Asia-Pasifiki".

Lin pia amesisitiza kuwa nchi zilizo nje ya kanda ya Asia-Pasifiki zinapaswa kuhehimu juhudi zilizofanywa na nchi za kanda hiyo katika kulinda amani na utulivu wa Bahari ya Kusini mwa China, badala ya kuchochea migogoro.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha