

Lugha Nyingine
Trump apiga marufuku raia wa nchi 12 kuingia Marekani
(CRI Online) Juni 05, 2025
Rais Donald Trump amesaini marufuku kamili ya kuingia Marekani dhidi ya raia wa nchi 12, ambazo ni Afghanistan, Myanmar, Chad, Jamhuri ya Kongo, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.
Rais Trump pia ametangaza vizuizi kadhaa vya kusafiri Marekani kwa raia wa nchi nyingine saba, ambazo ni Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistan na Venezuela.
Ikulu ya Marekani imesema hatua hizo zinalenga kulinda usalama wa Marekani.
Katika muhula wake wa kwanza wa urais Rais Trump aliwahi kusaini marufuku ya kuingia Marekani kwa raia wa Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, nchi saba zenye waislamu wengi, hatua ambayo ilizua malalamiko makubwa, na kudhaniwa kuwa ya kibaguzi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma