

Lugha Nyingine
Marais wa Marekani na Russia wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwenye mtandao wa kijamii kuwa amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Russia Vladimir Putin kwa muda wa dakika 75 jana Jumatano wakijadili migogoro kati ya Russia na Ukraine na suala la nyuklia la Iran.
Kwa mujibu wa Rais Trump, katika mazungumzo hayo, marais hao wawili wamezungumzia mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine dhidi ya Russia, na matukio mengine ya "kushambuliana kati ya nchi hizo mbili", huku Rais Putin akieleza kuwa Russia itajibu kithabiti tukio hilo la kushambuliwa kwa uwanja wake wa ndege.
Katika ujumbe wake Rais Trump ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ni "mazuri, lakini si yenye kuweza kuleta amani mara moja".
Kuhusu suala la nyuklia la Iran, Rais Trump ameeleza kuwa anadhani yeye na Rais Putin wanakubaliana kwamba Iran haitakiwi kumiliki silaha za nyuklia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma