

Lugha Nyingine
Wang Yi akutana na Mwenyekiti wa jumuiya ya JAPIT ya Japan
Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Mambo ya Nje, akikutana na Yohei Kono, mwenyekiti wa Jumuiya ya Japan ya Kuhimiza Biashara ya Kimataifa (JAPIT), mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 4, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
BEIJING - Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Mambo ya Nje ya China, amekutana na Yohei Kono, mwenyekiti wa Jumuiya ya Japan ya Kuhimiza Biashara ya Kimataifa (JAPIT), jana Jumatano mjini Beijing na kupongeza Kono kujitolea kwa muda mrefu kwa urafiki kati ya China na Japan na kusisitiza umuhimu wa mawasiliano kati ya watu katika hali ya sasa ya kimataifa.
Wang amesema kuwa China imetambua umuhimu wa kauli ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba kwamba Japan inapaswa kupata masomo ya kina kutoka kwenye historia na kujiepusha na kuwa nchi mvamizi.
Wang amesema kuwa historia haiwezi kubadilishwa, na kwamba ni kwa kujifunza tu kutoka kwenye historia ndipo pande zote mbili zinaweza kufungua mustakabali wa baadaye.
Kwa upande wake Kono amesema kuwa historia haiwezi kusahaulika, wala haipaswi kukataliwa, na ameongeza kuwa mambo yaliyopita hayawezi kubadilishwa lakini mambo ya baadaye yanaweza kuundwa kupitia juhudi za sasa.
“JAPIT inapenda kuendelea kuhimiza ushirikiano wa kirafiki kati ya Japan na China,” Kono amesema.
Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Mambo ya Nje, akikutana na Yohei Kono, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Japan ya Kuhimiza Biashara ya Kimataifa (JAPIT), mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 4, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma