

Lugha Nyingine
Rais Xi asema mazungumzo, ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa China na Marekani
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping katika mazungumzo ya simu jana Alhamisi yaliyofanyika kutokana na ombi la Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa mazungumzo na ushirikiano ndiyo chaguo pekee sahihi kwa China na Marekani.
Rais Xi amesema kuwa kurekebisha mwelekeo wa meli kubwa ya uhusiano kati ya China na Marekani kunahitaji pande hizo mbili kushika vizuri usukani na kupangilia njia sahihi, na hasa ni muhimu kujiepusha na misukosuko na mivurugo mbalimbali.
Xi amesemsa kuwa kwa pendekezo la upande wa Marekani, maofisa viongozi wa nchi hizo mbili hivi karibuni walifanya mkutano wa uchumi na biashara mjini Geneva, hiyo ilimaanisha hatua muhimu mbele katika kutatua masuala husika kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, na ilikaribishwa na jamii za nchi zote mbili na jumuiya ya kimataifa.
"Pande hizo mbili zinahitaji kutumia vizuri utaratibu uliokuwepo wa mashauriano kuhusu uchumi na biashara, na kutafuta maendeleo kwa pamoja zikiwa kwa moyo wa usawa, kunufaishana na kuheshimu ufuatiliaji wa kila upande," rais Xi alisema, na aliongeza kuwa upande wa China una udhati na kufuata kanuni.
Rais Xi alisema, Wachina siku zote wanaheshimu na kutekeleza kile ambacho kimeahidiwa, akihimiza pande zote mbili kutekeleza vizuri makubaliano yaliyofikiwa mjini Geneva.
"Hali halisi imeonesha kuwa, China imekuwa ikitekeleza makubaliano hayo kwa umakini na kwa dhati," Rais Xi ameongeza.
Amesema upande wa Marekani unapaswa kutambua maendeleo yaliyopatikana sasa, na kuondoa hatua hasi zilizochukuliwa dhidi ya China.
"Pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano katika mambo ya nje, sekta za uchumi na biashara, jeshi na utekelezaji wa sheria ili kujenga makubaliano, kuondoa sintofahamu na kuimarisha ushirikiano," Rais Xi ameongeza.
Rais Xi pia amesisitiza kuwa Marekani inapaswa kushughulikia suala la Taiwan kwa busara, ili kuepusha wafarakano wachache wanaotaka “Taiwan ijitenge” kuzivuta nchi mbili China na Marekani hadi kwenye hali hatari ya migogoro na mapambano. Kwa upande wake Rais Trump amesema kuwa anamheshimu sana Rais Xi, na uhusiano wa Marekani na China ni muhimu sana.
"Marekani inafurahia uchumi wa China kupata ongezeko kubwa, na Marekani na China zikifanya ushirikiano zinaweza kufanya mambo mengi mazuri," amesema.
Trump amesema Marekani itaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja.
"Mkutano wa Geneva ulikuwa wa mafanikio sana na ulileta makubaliano mazuri," alisema Trump, na aliongeza kuwa Marekani inapenda kufanya juhudi pamoja na China katika kutekeleza makubaliano hayo.
Rais Trump amesema Marekani inawakaribisha wanafunzi wa China wanaokuja kusoma Marekani.
Rais Xi amemkaribisha Trump kufanya ziara tena China, jambo ambalo Trump ameelezea shukrani zake za dhati.
Marais hao wawili wamekubaliana kwamba timu zao zinapaswa kuendelea kutekeleza makubaliano ya Geneva na kufanya duru nyingine ya mkutano haraka iwezekanavyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma