Wataalamu wa kilimo wa China watoa mafunzo ya kilimo cha mpunga nchini Guinea-Bissau

(CRI Online) Juni 06, 2025

Kundi la 12 la Ujumbe wa Usaidizi wa Kiufundi wa Kilimo wa China nchini Guinea-Bissau limetoa kozi ya mafunzo ya kilimo cha kisasa cha mpunga wenye kutoa mazao mengi katika mkoa wa Bafata, katikati ya nchi hiyo, ikilenga kuongeza uzalishaji wa nafaka na kuimarisha maendeleo ya kilimo.

Ikiwa imefanyika kuanzia Jumanne hadi jana Alhamisi, kozi hiyo, imehusisha hatua muhimu za ufundi wa kilimo cha mpunga kwa maofisa wa kilimo, wakulima, na mafundi kutoka sehemu mbalimbali za nchini humo.

Wataalamu hao wa China wametambulisha dhana jumuishi ya 'mbegu bora, hatua bora, na mbinu za hali ya juu,' ikihusisha maeneo mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mbegu, usimamizi wa mashamba, na udhibiti wa wadudu na magonjwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha