

Lugha Nyingine
Namibia kuimarisha uhusiano na China katika maonyesho ya uchumi na biashara
Namibia itatumia ushiriki wake katika Maonyesho ya Biashara na Uchumi kati ya China na Afrika (CAETE) yatakayofanyika Hunan, China, kuimarisha uhusiano wa kimkakati na kufungua fursa mpya za maendeleo.
Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi na Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Biashara ya nchini Namibia imesema, ushiriki wa nchi hiyo katika maonyesho hayo unaonyesha nia dhahiri ya kujenga uhusiano wa kimkakati na washirika wake wa maendeleo na bishara, ambao utafungua fursa kwa wananchi wake na kuiweka Namibia kuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya kikanda na bara la Afrika.
Kwa mujibu wa Wizara hiyo, Namibia itashiriki kama moja ya nchi mgeni wa heshima katika Maonyesho ya 4 ya Biashara na Uchumi kati ya China na Afrika yatakayofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 mwezi huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma