WFP yaishukuru China kwa msaada wake kwa waathirika wa majanga ya asili kusini mwa Madagascar

(CRI Online) Juni 06, 2025

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limeishukuru China kwa kutoa msaada muhimu wa chakula kwa zaidi ya watu 50,000 walioathiriwa na vimbunga vya kitropiki na majanga mengine ya tabianchi kusini mwa Madagascar.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano wiki hii, WFP imesema kuanzia Desemba mwaka 2024 hadi Machi mwaka huu, wafanyakazi wa China walisambaza tani 1,600 za mchele katika miji kadhaa ya kusini mwa Madagascar, na kuboresha usalama wa chakula katika maeneo yaliyo hatarini zaidi katika eneo hilo.

Akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya kukamilika kwa mradi husika wa msaada wa chakula iliyofanyika Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Balozi wa China nchini humo Bw. Ji Ping amesema, China itaendelea kushirikiana kwa karibu na Madagascar kutekeleza hatua mbalimbali za kukuza kilimo na kunufaisha wananchi, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana na kukabiliana kwa pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha