

Lugha Nyingine
China inayosonga mbele | Roboti "Xiao Tao" Asoma Katika Shule ya Mtandaoni (2)
![]() |
Hivi karibuni, kampuni moja ya roboti kutoka Jiangsu, China, iliamua kuipeleka "Xiao Tao", roboti iliyotengenezwa nao wenyewe, kusoma shuleni huko Hangzhou, China. Shule hiyo si ya kawaida, bali ni jukwaa la kidijitali linalowafundisha roboti kuelewa na kuchangamana na mazingira, likitolewa na kampuni ya Manycore Tech.
Katika mazingira ya kidijitali, "Xiao Tao" anajifunza kazi kama kufunga na kufungua milango ya jokofu, au kuchukua kikombe cha maziwa.
Tang Rui, mwanasayansi mkuu wa Manycore Tech alisema kuwa, kazi hizi ni ngumu sana kwa roboti, kwa kuwa zinahitaji udhibiti sahihi wa mwendo na uelewa wa kina wa nafasi.
Kwa sasa kampuni ya Manycore Tech imekusanya mamilioni ya miundo ya 3D, ambayo inawezesha roboti kujifunza haraka na kwa gharama nafuu zaidi kupitia mafunzo ya mtandaoni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma