

Lugha Nyingine
Miradi ya kuzalisha umeme kwa maji iliyojengwa na kampuni ya China yakuza maendeleo ya watu wenye ujuzi nchini Cote d'Ivoire
![]() |
Picha iliyopigwa Mei 28, 2025 ikionyesha Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Gribo-Popoli mjini Soubre, Cote d'Ivoire. (Xinhua/Wang Guansen) |
ABIDJAN - Msimu wa mvua unapoanza kusini-magharibi mwa Cote d'Ivoire, Mto Sassandra umejaa kwa uhai mpya. Kwenye ukungu wa mapema asubuhi, wafanyakazi waliovaa sare na kofia wanasogea kupitia Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Gribo-Popoli, kukagua njia za kumwaga maji, kufuatilia viwango vya maji, na kukagua vifaa.
Miongoni mwao ni Bassirou Konate mwenye umri wa miaka 32, mkaguzi ubora ambaye alianza kazi yake hiyo muongo karibu mmoja uliopita.
"Nilipojiunga kwa mara ya kwanza na mradi huu wa kuzalisha umeme uliojengwa na China, sikuweza kusoma ramani," Konate amekumbushia. "Lakini mshauri Mchina alipangwa kufanya kazi nami. Hatua kwa hatua, alinifundisha kila kitu."amesema.
Konate alianza kazi yake mwaka 2016 katika Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Soubre, mradi uliojengwa pia na Shirika la Ujenzi wa Nishati la China (PowerChina). Tangu wakati huo, amekuwa akishiriki katika mipango kadhaa mikuu ya miundombinu na kuwa sehemu muhimu ya timu inayojenga Kituo cha kuzalisha umeme cha Gribo-Popoli.
"Nilichojifunza shuleni kilikuwa nadharia. Ni miradi hii ambayo ilinipa uzoefu wa vitendo. Sasa, ninaweza kuunga mkono familia yangu. Ninaona mustakabali si tu kwa ajili yangu mwenyewe bali kwa jamii yangu", Amesema.
Kikiwa kinapatikana kwenye moja ya mito mikuu ya Cote d'Ivoire, kituo hicho cha Gribo-Popoli ni sehemu ya miradi ya kuzalisha umeme kwa maji. Mto Sassandra, ukiwa na mtiririko wake mwingi wa maji na miinuko inayofaa, una uwezo mkubwa wa nishati mbadala.
Baada ya kukamilisha Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Soubre mwaka 2017, PowerChina ilishuhudia vitengo vyote vitatu vya kuzalisha umeme vya Gribo-Popoli vikianza uzalishaji kufikia Novemba mwaka 2024, ikifungua uwezo zaidi wa kuzalisha umeme kwa maji nchini humo.
Hata hivyo, nishati ambayo miradi hiyo inazalisha ni zaidi ya umeme -- pia inawezesha ukuaji wa vipaji vya wenyeji.
Wafanyakazi wengi wa Cote d’Ivoire ambao walianza kazi zao katika eneo hilo la Soubre, kama Konate, tangu wakati huo wameingia katika majukumu muhimu kwenye mradi wa Gribo-Popoli wakiwa wakaguzi ubora, mafundi na wasimamizi. Utaalam wao unaokua unawezesha ukurasa mpya wa nchi hiyo katika ujenzi wa miundombinu, ile inayoendeshwa si tu na mashine, lakini kwa mikono yenye ujuzi ya wataalamu wenyeji.
Hou Bing, mhandisi mkuu wa kituo cha Gribo-Popoli, anasema mradi huo umetoa ajira takriban 2,000 za moja kwa moja wakati wa awamu yake ya ujenzi na kuunga mkono ajira 1,000 nyingine kupitia sekta zinazohusiana.
"Miradi hii ni zaidi ya maeneo ya kazi. Ni shule, mahali ambapo wafanyakazi wa Cote d’Ivoire wanapata ujuzi na kujiamini. Maarifa yanapitishwa pamoja na kuaminiana kati ya watu wetu. Kwa pamoja, tunajenga si tu mabwawa lakini madaraja ya urafiki." Hou amebainisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma