Rais Xi Jinping apokea ziara ya Panchen Rinpoche (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2025
Rais Xi Jinping apokea ziara ya Panchen Rinpoche
Panchen Erdeni Chos-kyi rGyal-po akikabidhi hada kwa Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), katika Zhongnanhai mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 6, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China Ijumaa alitoa wito kwa Panchen Rinpoche wa Ubuddha wa Kitibet kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza umoja wa kikabila na masikilizano ya kidini, vilevile utulivu, maendeleo katika Mkoa unaojiendesha wa kabila la Watibet wa Xizang, kusini magharibi mwa China.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo alipokuwa akipokea ziara ya Panchen Erdeni Chos-kyi rGyal-po katika Zhongnanhai mjini Beijing.

Katika ziara hiyo, Panchen Rinpoche amemkabidhi Rais Xi hada, skafu ya kijadi ya hariri ya Tibet ambayo ni ishara ya usafi usio na doa na baraka, na kumfahamisha rais juu ya masomo na kazi yake katika miaka ya hivi karibuni.

Akimpongeza Panchen Rinpoche kwa hatua alizopiga katika mambo mbalimbali, Rais Xi ameeleza matumaini yake kwamba Panchen Rinpoche ataenzi mila tukufu ya Ubudha wa Tibet katika kupenda nchi, na bila kuyumba yumba kulinda umoja wa kitaifa na mshikamano wa kikabila.

Rais Xi ametoa wito kwa Panchen Rinpoche kuzidisha kila mara masomo yake ya kidini na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga hisia thabiti ya jumuiya kwa taifa la China, kwa utaratibu kuendeleza kanuni ya kidini nchini China yenye umaalum wa China, na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa mkoani Xizang.

Panchen Rinpoche amesema atashikilia bila kuyumbma yumba uongozi wa CPC, kithabiti kulinda umoja wa kitaifa na mshikamano wa kikabila, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuimarisha mshikamano na maendeleo ya kikabila, kuhakikisha kwamba dini nchini humo lazima ziwe na umaalum wa China, na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa mkoani Xizang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha