Kiongozi wa Myanmar asema angependa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya Myanmar na China yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2025
Kiongozi wa Myanmar asema angependa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya Myanmar na China yenye mustakabali wa pamoja
Kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Myanmar na China mjini Nay Pyi Taw, Myanmar, Juni 8, 2025. (Xinhua/Myo Kyaw Soe)

NAT PYI TAW, Myanmar – Hafla ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Myanmar imefanyika jana Jumapili mjini Nay Pyi Taw, Myanmar, ambapo katika hotuba yake, kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing amesema kuwa Myanmar inapenda kushirikiana bega kwa bega na China, kuendelea kithabiti kufanya juhudi katika kuimarisha uhusiano wa "Paukphaw" (kindugu) wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili na kuendelea na juhudi zake za kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya Myanmar na China yenye mustakabali wa pamoja.

Min Aung Hlaing amesema kuwa Myanmar na China kwa muda mrefu zimekuwa zikifurahia jadi ya uhusiano wa karibu, wa kirafiki na wa ujirani mwema pamoja na moyo wa "Paukphaw".

"Katika kipindi cha miaka 75 iliyopita ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Myanmar na China, uhusiano wa kirafiki kati ya serikali mbili, watu na sekta mbalimbali za kijamii umeendelea kustawi kwa kasi. Ushirikiano katika sekta muhimu, zikiwemo za uwekezaji na biashara, umepata maendeleo makubwa," amesema.

Amesema, Myanmar na China zinafungamana na dhamira ya kina na ya kudumu ya Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani, msingi wa uhusiano wao na kielelezo cha uhusiano wa kisasa wa kimataifa.

"Myanmar itaendelea kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inakaribisha Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia, na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia," amesema.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Myanmar Ma Jia amesema kuwa China na Myanmar zimeunganishwa na milima na mito, na mawasiliano yao ya kirafiki yanachukua maelfu ya miaka.

"Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya China na Myanmar siku zote umekuwa thabiti kama mwamba. Mustakabali ya nchi hizo mbili imeunganishwa kwa ukaribu. Nchi hizo mbili zinaendelea kufungua kurasa mpya za urafiki wao wa kindugu katika nyanja mbalimbali," Ma amesema.

Ma amesema kuwa China itatafuta ujirani wenye amani, salama na ustawi, kufuata kanuni ya urafiki, udhati, kunufaishana na ujumuishaji, na kuwa pamoja dhiki na faraja na majirani zake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha