Mlinzi wa kulungu milu ajitolea kutafuta mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2025
Mlinzi wa kulungu milu ajitolea kutafuta mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili
Picha iliyopigwa tarehe 7 Juni, 2025, ikionyesha Kulungu Milu akipita maji kwenye Hifadhi ya taifa ya mazingira ya asili ya Milu ya Dafeng, mkoani Jiangsu, mashariki mwa China. (Xinhua/Sun Fanyue)

Xue Dandan, mwenye umri wa miaka 35, ni mkuu wa idara ya usalama ya Hifadhi hiyo. Baada ya kuhitimu masomo mwaka 2016, alijitolea katika usimamizi wa doria na elimu ya sayansi ya umma ya kulungu milu katika hifadhi hiyo.

Wakati alipofika mara ya kwanza, alijua kidogo kuhusu mnyama huyu. Katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, Xue amezamia katika mambo husika, akitafuta ushauri wa wataalam na wasomi, na kufanya doria za mara kwa mara na wenzake. Huku akiboresha ujuzi wake kuhusu mnyama huyu kila mara, pia amegeuza ujuzi wa kitaalamu wa ulinzi wa kulungu milu hao kuwa taarifa zinazoweza kufikiwa na umma.

Kupitia kazi ya kila siku, Xue amejenga uhusiano mkubwa na kulungu milu. Amesaidia wanakijiji kuokoa kulungu milu walionaswa na nyavu, na pia ameshiriki katika kujenga jukwaa la kisasa, ambalo linafuatilia bioanuwai ya makazi ya kulungu milu. "Hifadhi ni kama nyumba yangu na kulungu milu ni familia yangu," amesema.

Mwaka 1986, Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Milu ya Dafeng ilileta kulungu milu 39 kutoka Uingereza. Katika miaka ya hivi karibuni, ikijita katika kuhimiza kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili, hifadhi hiyo imekuza mimea inayostahimili chumvi-alkali na kudhibiti mimea vamizi. Kadiri mfumo wa ikolojia unavyozidi kuboreka, idadi ya kulungu milu imekuwa ikiongezeka kwa kasi. Hadi kufikia Juni 2024, hifadhi hiyo ilikuwa na kulungu milu zaidi ya 8,200, ikiwemo idadi ya kulungu milu wa mwituni zaidi ya 3,500.

Kwa Xue, lengo kuu la kazi yake ni kurejesha idadi ya kulungu milu wa mwituni. Yeye na wenzake wanaendelea na juhudi zao katika uhifadhi wa kuhamisha wanyama kwenda maeneo mengine, kuwapeleka kwenye makazi yanayofaa. Xue anaamini kwamba hii ni njia muhimu kuelekea kufikia kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha