

Lugha Nyingine
Bandari mpya iliyojengwa na China yaunganisha zamani, sasa na siku za baadaye nchini Tanzania (3)
![]() |
Watu wakifanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa inayoendelea kujengwa karibu na Kilwa Kisiwani, Tanzania, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Li Yahui) |
DAR ES SALAAM - Upepo mwanana wa baharini ulikuwa ukitikisa miti kwenye kisiwa tulivu karibu na pwani ya kusini mashariki mwa Tanzania. Hapa kuna magofu ya Kilwa Kisiwani, iliyokuwa bandari yenye shughuli nyingi kwenye njia ya biashara ya Bahari ya Hindi, ambapo meli zilizosheheni dhahabu, viungo vya chakula na kaure zilikuwa zikikusanyika kwa wingi.
Sasa, katika ng'ambo tu ya habari, bandari nyingine inaanza kuonekana. Bandari ya Uvuvi ya Kilwa, ambayo pia imepewa jina la "bandari ya siku za baadaye," inajengwa.
Gati lenye urefu wa mita 315 linaenea ndani ya bahari kama mkono wa chuma. Karibu na hapo, ujenzi unaendelea kwa kasi kwenye mradi wa kuhifadhia bidhaa za mnyororo baridi, soko la biashara, majengo ya ofisi, na mtambo wa kushughulikia maji taka. Bandari hiyo mpya inatarajiwa kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa miaka mingi ijayo.
Rekodi za kihistoria zinaonyesha kwamba baharia wa China Zheng He aliongoza meli kubwa wakati wa Enzi ya Ming (1368-1644 BK) katika safari saba za Bahari ya Hindi, akifika mbali hadi Afrika Mashariki na Bahari Nyekundu.
"Vipande vingi vya kaure za China vimefukuliwa katika eneo la Kilwa Kisiwani. Inaonyesha ni muda mrefu kiasi gani urafiki kati ya Tanzania na China umekuwepo," amesema Shomari Rajabu Shomari, mtunza historia wa Makumbusho ya Taifa ya Tanzania.
"Miaka mia sita iliyopita, Wachina walikuja kwa amani kufanya biashara. Sasa, miaka mia sita baadaye, wanatusaidia kujenga bandari ambayo inaongoza kuelekea ustawi," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano, akionyesha chati ya zamani ya kundi la meli za China za karne ya 15.
Mradi huo, unaojengwa na Kampuni ya China ya Uhandisi wa Bandari (CHEC), kampuni ongozi ya ujenzi ya China, ni bandari ya kwanza ya kisasa ya uvuvi nchini Tanzania.
Ikiwa inachukua eneo lenye ukubwa wa hekta takriban 5.6, imeundwa kushughulikia tani 60,000 za samaki kwa mwaka na inaweza kuwezesha meli za uvuvi kwenye kina kirefu cha bahari kutia nanga, kwa mujibu wa na Chen Zhifeng, makamu meneja wa mradi wa idara ya mradi wa baharini ya CHEC Tawi la Tanzania. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba.
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alihudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi mwaka 2023, akisisitiza umuhimu wa bandari hiyo kwa uchumi wa taifa na maisha ya watu.
"Baada ya kukamilika, miradi ya kuhifadhia bidhaa za mnyororo baridi na biashara vitatatua tatizo la uhifadhi. Wavuvi hawatakuwa na wasiwasi kuhusu samaki ambao hawajauzwa, na uvuvi kwenye bahari kuu pia utawezekana," amesema Chen.
Kwenye eneo la ujenzi, ajira karibu 600 za moja kwa moja zimeundwa, zikiwa ni pamoja na wachomeleaji, waendeshaji kreni na madereva wa mashine za kuchimba.
"Kila mhandisi wa China anashauri na kulea vipaji vya wafanyakazi wa Tanzania takriban makumi na zaidi, mara kwa mara akiwaamini kufanya kazi kwa kujitegemea. Mbinu hii ya mafunzo imeongeza ujuzi wa kiutendaji wa wafanyakazi wenyeji," amesema Edwin Christopher, meneja wa rasilimali watu na usimamizi wa mradi huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma