Kijiji cha Heitu Kusini mwa China chaanzisha ushirika kuendeleza vyombo vya ufinyanzi vya Kabila la Wali (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2025
Kijiji cha Heitu Kusini mwa China chaanzisha ushirika kuendeleza vyombo vya ufinyanzi vya Kabila la Wali
Mwanakijiji Dong Jiajia akiuza vyombo vya ufinyanzi wa udongo wa kabila la Wali kwa kutangaza moja kwa moja mtandaoni kwenye ushirika wa ufinyanzi katika Kijiji cha Heitu cha Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Juni 9, 2025. (Xinhua/Zhang Liyun)

Ukiwa ni mali ya urithi wa kitaifa wa utamaduni usioshikika wa China, ufundi na ustadi wa kufinyanga vyombo vya udongo wa Kabila la Wali unabeba hekima na kumbukumbu ya kiutamaduni ya kabila hilo.

Katika Kijiji cha Heitu cha Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, kuanzishwa kwa ushirika wa ufinyanzi wa udongo kumetoa njia mpya kwa wanakijiji wenyeji kurithisha ufundi na ustadi huo wa kufinyanga vyombo vya udongo na kuuza bidhaa zao za ufinyanzi.

Shukrani kwa juhudi za kunadi bidhaa za ushirika huo, kazi hizo za ufinyanzi za watu wa Kabila la Wali zimekuwa alama ya kiutamaduni ya Kijiji cha Heitu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha