Safari ya Swala wa Tibet ya kuhama kwenda kuzaa katika Mkoa wa Xizang, China yaendelea (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2025
Safari ya Swala wa Tibet ya kuhama kwenda kuzaa katika Mkoa wa Xizang, China yaendelea
Swala wa Tibet wakiwa katika safari ya kuhama katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Asili ya Changtang, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, tarehe 10 Juni, 2025. (Xinhua/Liu Jinhai)

LHASA - Kila mwaka, swala wajawazito wa Tibet katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China wanaanza uhamaji wao wa mwaka kwenda kujifungua kati ya miezi ya Mei na Julai. Maadui wao wa asili wakiwemo mbwa mwitu na dubu muda wote huwa wapo kuwavizia. Hata hivyo, Swala wengi kati yao wanaweza kufanikiwa kuepusha hatari na kuzaa watoto.

Idadi ya swala wa Tibet katika mkoa huo wa Xizang sasa imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 300,000, na hadhi yao ya ulinzi imeshushwa kutoka "kuwa hatarini kutoweka" hadi "kuwa karibu na kutishiwa," takwimu kutoka idara ya ikolojia na mazingira ya mkoa huo zinaonesha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha