Barabara Kuu ya Lingyuan-Suizhong yaendelea kujengwa katika Mkoa wa Liaoning, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2025
Barabara Kuu ya Lingyuan-Suizhong yaendelea kujengwa katika Mkoa wa Liaoning, China
Picha ya droni iliyopigwa tarehe 12 Juni 2025 ikionyesha ujenzi unaoendelea wa sehemu ya barabara ya mwendo kasi ya Lingyuan-Suizhong katika Wilaya ya Jianchang ya Mji wa Huludao wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing)

Ujenzi wa sehemu ya Barabara ya mwendo kasi ya Lingyuan-Suizhong unaendelea kufanyika katika Wilaya ya Jianchang ya Mji wa Huludao wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China. Baada ya kukamilika, barabara hiyo itaboresha hali ya mawasiliano katika sehemu ya magharibi ya Mkoa wa Liaoning na mashariki mwa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani. Pia itatoa mchango muhimu katika kustawisha kituo cha viwanda vilivyoanzishwa zamani kaskazini mashariki mwa China, na kuhimiza ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya pembezoni mwa barabara hiyo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha