Xinjiang, kituo muhimu cha kupeleka umeme katika mpango wa usambazaji nishati wa China kutoka magharibi hadi mashariki (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2025
Xinjiang, kituo muhimu cha kupeleka umeme katika mpango wa usambazaji nishati wa China kutoka magharibi hadi mashariki
Picha iliyopigwa Julai 6, 2025 ikionyesha njia za umeme za mradi wa kusafirisha umeme wa nguvu ya juu ya ±1100 kV kwa mkondo wa moja kwa moja wa Changji-Guquan katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wakazak ya Mori, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Picha na Zhang Limin/Xinhua)

Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China ni kituo kikuu cha kupelekea umeme cha mradi wa China wa kusafirisha umeme kutoka eneo la magharibi hadi mashariki.

Awali eneo kubwa la jangwa na ardhi kame mkoani Xinjiang vilichukuliwa kuwa vizuizi vya uchumi wa mkoa huo, lakini sasa vimebadilishwa kuwa "mgodi wa dhahabu" wa nishati mbadala, ambapo kuna upepo mkali na mwanga wa jua wa saa nyingi.

Tangu mwaka 2010, mkoa huo wa Xinjiang kwa ujumla umesafirisha umeme zaidi ya saa za kilowati bilioni 900 kwa nje ya mkoa huo, kati yake nishati mbadala ikichukua takriban asilimia 30 ya jumla ya nishati hiyo. Umeme wake unapelekwa na kufika hadi maeneo 22 ya ngazi ya mikoa nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha