

Lugha Nyingine
Xinjiang, kituo muhimu cha kupeleka umeme katika mpango wa usambazaji nishati wa China kutoka magharibi hadi mashariki
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2025
Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China ni kituo kikuu cha kupelekea umeme cha mradi wa China wa kusafirisha umeme kutoka eneo la magharibi hadi mashariki.
Awali eneo kubwa la jangwa na ardhi kame mkoani Xinjiang vilichukuliwa kuwa vizuizi vya uchumi wa mkoa huo, lakini sasa vimebadilishwa kuwa "mgodi wa dhahabu" wa nishati mbadala, ambapo kuna upepo mkali na mwanga wa jua wa saa nyingi.
Tangu mwaka 2010, mkoa huo wa Xinjiang kwa ujumla umesafirisha umeme zaidi ya saa za kilowati bilioni 900 kwa nje ya mkoa huo, kati yake nishati mbadala ikichukua takriban asilimia 30 ya jumla ya nishati hiyo. Umeme wake unapelekwa na kufika hadi maeneo 22 ya ngazi ya mikoa nchini China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma