

Lugha Nyingine
CPI ya China yarudi juu huku kukiwa na sera zinazounga mkono matumizi (4)
![]() |
Mteja (kulia) akifanya manunuzi kwenye duka la simu mjini Binzhou, Mkoani Shandong, mashariki mwa China, Julai 9, 2025. (Picha na Chu Baorui/Xinhua) |
BEIJING - Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) imesema, kiwango cha bei ya vitu vya watumiaji cha China (CPI), ambacho ni kiwango kikuu cha mfumuko wa bei, kilipanda kwa asilimia 0.1 mwezi Juni kuliko mwaka jana, wakati ambapo hatua za nchi hiyo zinazolenga kupanua mahitaji ya ndani na kuimarisha bei za bidhaa za matumizi za viwandani zikiunga mkono kupanda kwa bei.
Katika takwimu zake zilizotolewa jana Jumatano, NBS imesema kuwa kiwango cha CPI katika maeneo ya mijini kilipanda kwa asilimia 0.1 mwezi uliopita kuliko mwaka jana, wakati kile cha maeneo ya vijijini kilipungua kwa asilimia 0.2.
"Ongezeko la asilimia 0.1 la CPI mwezi Juni pia lilibadilisha mwelekeo wa kushuka kwa kiwango hicho kwa miezi minne mfululizo," amesema mtakwimu wa NBS Dong Lijuan.
Dong amehusisha kupanda kwa bei hasa na kuimarika kwa bei za bidhaa za matumizi za viwandani, ambazo zilishuhudia kushuka kwa bei kukiendelea kupungua mwezi Juni, ikisababisha kupungua shinikizo kwa CPI.
Kwa mfano, takwimu hizo zinaonyesha kuwa, kupanda kwa bei ya mafuta mwezi uliopita kulipunguza shinikizo la kushuka kwa bei ya nishati kwenye CPI na kwamba kuimarika huko kwa bei ya mafuta pekee kulishuhudia athari zake kwa CPI zikipungua zaidi kwa asilimia 0.08 mwezi Juni ikilinganishwa na mwezi uliopita.
"Athari za sera za serikali za kuongeza matumizi zimeendelea kuonekana," Dong amesema, akirejelea ongezeko la bei za bidhaa za matumizi ya kiutamaduni na burudani na vifaa vya umeme vya matumizi ya nyumbani, ambavyo vilishuhudia bei zao zikipanda kwa asilimia 2 na asilimia 1 mtawalia, mwezi Juni.
Kiwango kikuu cha CPI, ambacho hakijumuishi bei za chakula na nishati, kilipanda kwa asilimia 0.7 mwezi Juni, ongezeko la asilimia 0.1 ikilinganishwa na ongezeko la mwezi Mei, kwa mujibu wa NBS.
"Kiwango kikuu cha CPI pia kilirekodiwa kiwango chake cha juu zaidi katika miezi 14," Dong amesema.
Takwimu hizo za Jumatano pia zimeonyesha kuwa kiwango cha bei ya wazalishaji wa China (PPI), ambacho hupima gharama za bidhaa kutoka kiwanda, kilishuka kwa asilimia 3.6 mwezi Juni, punguo hilo limeongezeka kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na takwimu za PPI za mwezi Mei.
PPI ilishuka kwa asilimia 0.4 mwezi Juni kuliko mwezi uliopita. Katika nusu ya kwanza ya 2025, PPI ilipungua kwa asilimia 2.8 kuliko mwaka uliopita wakati kama huo, kwa mujibu wa takwimu hizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma