

Lugha Nyingine
Makumbusho ya vijiji vya kale visivyo na kuta za mipaka katika Wilaya ya Jinxi, China (4)
Wilaya ya Jinxi, katika Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China yenye historia ya karne nyingi, bado inahifadhi vijiji vya kale zaidi ya 100 vyenye historia inayoanzia enzi za Ming na Qing (1368-1911), hali ambayo imeipa umaarufu wilaya hiyo wa kuwa "makumbusho ya vijiji vya kale bila kuta za mipaka." Kijiji cha Zhuqiao ni mwakilishi mashuhuri miongoni mwa vijiji hivyo, kikiwa na majengo 109 ya kale yaliyopo hadi sasa kutoka enzi hizo za Ming na Qing.
Ili kuenzi mambo yake ya kale, mamlaka za serikali za mitaa zimekuwa zikiboresha kila mara miundombinu katika kijiji hicho cha Zhuqiao, kukarabati majengo ya kihistoria kwa utaratibu, na kujikita katika kuendeleza viwanda kama vile ubunifu wa kitamaduni, huduma za afya za dawa za jadi za Kichina, na nyumba za wageni zenye umaalumu.
Mwaka 2024, kijiji hicho cha Zhuqiao kilipokea wageni takriban 514,300, na kuzalisha yuan zaidi ya milioni 3 (dola za Kimarekani kama 418,018) kama mapato ya ziada kwa wanakijiji wenyeji, kikijiweka kama mfano wa kuigwa wa ustawishaji wa kijiji cha kale ambacho kinafungamanisha kujionea mambo ya kitamaduni, utafiti wa urithi wa utamaduni usioshikika, na utalii wa kijijini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma