

Lugha Nyingine
Wafanyakazi wavumilia hali yenye changamoto mno jangwani kukamilisha "njia ya mwendokasi ya umeme" kusini mwa Xinjiang, China (2)
China imekamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa nguvu ya juu zaidi yenye urefu wa kilomita 4,197 kuzunguka Bonde la Tarim, ambalo ni sehemu ya jangwa kubwa zaidi la China, ikionesha maendeleo makubwa katika eneo la kusini la Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang.
Kampuni tanzu ya Shirika la Gridi ya Kitaifa la China ya Xinjiang Electric Power ambayo imejenga mradi huo ikisema, Sehemu ya mwisho ya njia hiyo ya umeme wa nguvu ya kilovolti 750 (kV), ambayo sasa ni kubwa zaidi ya aina yake kwa China, imeunganishwa rasmi jana Jumapili, ikikamilisha ujenzi wa mradi huo wa miaka 15 unaohusisha vituo tisa vya kupozea umeme na minara ya chuma karibu 10,000.
Njia hiyo ya kusambaza umeme inapitia ardhi ya hali tofauti kubwa kabisa kutoka mchanga wa jangwani unaohamahama hadi miinuko ya juu ya Milima ya Kunlun.
Chen Lin, mmoja wa wafanyakazi wajenzi wa ujenzi wa njia hiyo, mwezi Machi mwaka huu aliwasili katika sehemu ya ukingo wa kusini wa Jangwa la Taklimakan, ambapo yeye na wenzake zaidi ya 40 wakishirikiana bega kwa bega, wamekamilisha sehemu ya kazi ya ujenzi wa njia hiyo ya kusafirisha umeme kwa kukabiliwa na upepo wa mchanga na joto kali kabisa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma