Bohari Kongwe la Mafuta lafungamanisha Usanifu wa Kiviwanda na Burudani mkoani Hunan, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2025
Bohari Kongwe la Mafuta lafungamanisha Usanifu wa Kiviwanda na Burudani mkoani Hunan, China
Picha iliyopigwa Julai 13, 2025 ikionesha bohari kongwe la mafuta lisilotumika mjini Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China, Julai 13, 2025. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Katika wilaya ya Tianxin ya Mji wa Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China matangi 12 makongwe ya mafuta yasiyotumika yanasimama kando ya Mto Xiangjiang. Eneo hilo awali lilitumika kama bohari la mafuta kwa ajili ya mji huo, na kwa kiasi kikubwa liliachwa bila kutumika kuanzia miaka ya 1990.

Mwezi huu wa Julai umeshuhudia kufunguliwa upya kwa eneo hilo la urithi wa kiviwanda, huku matangi hayo ya mafuta na miundombinu yake saidizi vikigeuzwa kuwa mikahawa yenye kuvutia, kumbi za maonesho, maduka ya sanaa, miongoni mwa mambo mengine, likijumuisha mfungamano kati ya usanifu wa kiviwanda na burudani mbalimbali za wateja ambavyo vinavutia wote wakazi na watalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha