Kutembelea "Dirisha la Paa" wa asili kwenye pango la Mlima Jinzhong, Guangxi, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2025
Kutembelea
(Picha na Lei Qijun/People's Daily Online)

Ukitembea kwenye pango tulivu na kupitia ushoroba wa kiajabu kwenye Mlima Jinzhong huko Guilin, unaweza kuona "dirisha la paa" (skylight) wa asili juu ya pango, ambapo jua huangaza kwa ndani kimshazari, likiwasilisha mwanga wa kupendeza sana.

"Dirisha la paa" hilo liko katika Eneo la Kivutio cha Utalii la Mlima Jinzhong katika Mji mdogo wa Luojin wa Mji wa Guilin, Mkoa wa Guangxi, China. Wakati jua linapoangaza kupitia tundu hilo na kuingia kwenye pango, tukio liitwalo “Tyndall effect” hutokea, likiwafanya watu wahisi kama kuwa katika nchi ya vichimbakazi. Muonekano huo unaonesha maajabu ya mazingira ya asili na mvuto wa mandhari ya Guilin, na pia umekuwa ukivutia idadi kubwa ya watalii kupiga picha na kuweka maudhui yake mtandaoni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha