Wasanii wa Mongolia ya Ndani wawasilisha nyimbo na ngoma za Kichina nchini Ethiopia (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2025
Wasanii wa Mongolia ya Ndani wawasilisha nyimbo na ngoma za Kichina nchini Ethiopia
Msanii wa Mongolia ya Ndani akicheza ngoma mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, tarehe 13 Julai 2025. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Kundi la wasanii kutoka Mongolia ya Ndani, mkoa wa kaskazini mwa China, wamewasilisha onyesho la nyimbo na ngoma za kijadi na za kisasa mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Jumapili jioni.

Shughuli hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Ethiopia na Wizara ya Utamaduni na Michezo ya Ethiopia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ethiopia.

Onyesho hilo limefanyika kwenye jengo la makao makuu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia, ambalo lilijengwa na kampuni ya China, pia ni jengo refu zaidi Afrika Mashariki.

Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utamaduni na Michezo wa Ethiopia Nebiyou Baye amesema uhusiano wa kidiplomasia na wa kiuchumi wa muda mrefu na wa mambo mengi kati ya nchi hizo mbili umestawi na kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

"Sasa, uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ethiopia na China unaitwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote, hasa katika masuala ya utamaduni, sanaa na michezo. Uhusiano huo umeendelezwa na kuonyeshwa kwa namna mbalimbali," Baye amesema.

Waziri huyo wa nchi amesema wasanii hao wameleta onyesho la kuvutia kwa waethiopia, wakionyesha tamaduni na mila tajiri za China.

"Ni onyesho la kuvutia sana. Tumeweza kujionea maonyesho kutoka mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, na maonyesho ya wasanii yanastaajabisha na ya kushangaza. Baadhi ya maonyesho yameorodheshwa kama urithi wa binadamu na UNESCO," Baye amesema.

Kwa mujibu wa waziri huyo, wasanii wa Ethiopia watakuwa wakisafiri na kufanya maonyesho katika sehemu tofauti za China hivi karibuni na mawasiliano hayo ya kisanii yanatarajiwa kuimarisha uhusiano wa hali zote wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kufuatia kuinuliwa hadhi ya uhusiano wao kuwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote mwaka 2023, China na Ethiopia zimeimarisha zaidi ushirikiano wao wa sekta mbalimbali katika mwaka 2024 na 2025 kwa kuongezwa kwa mawasiliano ya kidiplomasia na ya ngazi ya juu, ushirikiano thabiti wa kibiashara na kiuchumi, na uendelezaji ipasavyo wa uwezo na uhamishaji maarifa.

Onyesho hilo la Jumapili lilivutia watu zaidi ya 700, wakiwemo maafisa wa serikali ya Ethiopia na wasanii, na watu wa jamii ya Wachina mjini Addis Ababa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha