Bustani ya Wanyama ya Chongqing, China yachukua hatua kusaidia wanyama kukwepa joto kali la majira ya joto (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2025
Bustani ya Wanyama ya Chongqing, China yachukua hatua kusaidia wanyama kukwepa joto kali la majira ya joto
Dubu mweusi akicheza na mchemraba wa barafu kwenye Bustani ya Wanyama ya Chongqing, kusini-magharibi mwa China, Julai 16, 2025. (Xinhua/Tang Yi)

Huku hali ya Hewa ya joto kali ikiendelea katika Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China, Bustani ya Wanyama ya Chongqing imechukua hatua mbalimbali ili kuwasaidia wanyama kukwepa joto kali la majira ya joto, zikiwemo za kuwapa maji ya kuogelea ya barafu, kuwapa kiyoyozi, na kuwalisha vyakula vyenye barafu. Yote haya yanalenga kuhakikisha usalama na faraja zao katika majira mazima ya joto.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha