Waziri wa Biashara wa Lesotho asema ushuru uliowekwa na Marekani hauna usawa kwa nchi zinazoendelea

(CRI Online) Agosti 04, 2025
Waziri wa Biashara wa Lesotho asema ushuru uliowekwa na Marekani hauna usawa kwa nchi zinazoendelea
Mokhethi Shelile, waziri wa maendeleo ya Biashara, Viwanda, na Utalii wa Lesotho, akiongea wakati wa mahojiano na Xinhua, Shirika la Habari la China huko Maseru, Lesotho, Julai 29, 2025. (Xinhua/Wang Guansen)

Waziri wa maendeleo ya Biashara, Viwanda, na Utalii wa Lesotho, Mokhethi Shelile amesema, ushuru uliowekwa na Marekani hauna usawa kwa nchi zinazoendelea kama Lesotho, na umekuwa pigo kubwa kwa sekta ya nguo ya nchi hiyo.

Amesema huduma kama vibali kutoka Microsoft ambacho Lesotho inalipia mamilioni ya dola kwa mwaka havikuzingatiwa na Marekani, na kuongeza kuwa, baadhi ya bidhaa za Marekani zinaingia nchini Lesotho kupitia Afrika Kusini na vinaondolewa kimakosa katika hesabu ya bidhaa zinazoingizwa nchini humo.

Ameonya kuwa, upotevu wa ajira kutokana na ushuru uliowekwa na Marekani utakuwa na athari kubwa katika sekta nyingine kama usafiri na nyumba, na hivyo kuwa tishio la kukosekana kwa utulivu wa kijamii.

Lesotho ni moja ya nchi za Afrika inayouza kwa wingi vitambaa nchini Marekani, pia ni moja ya nchi masikini zaidi duniani, na sekta yake ya nguo ni msingi mkuu wa uchumi wake na ajira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha