

Lugha Nyingine
Wataalamu waonya mgawanyiko wa Sudan wakati juhudi za amani zikikwama
Wachambuzi wameonya kuwa, mgogoro wa Sudan una hatari ya kuleta mgawanyiko usioweza kusuluhishwa, wakati juhudi za kidiplomasia zikishindwa na mgawanyiko wa ndani ukiongezeka.
Mpaka sasa, Jeshi la Sudan limepata mafanikio makubwa katika maeneo ya mashariki na katikati ya Sudan, likichukua udhibiti wa maeneo muhimu ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, wakati RSF likidhibiti sehemu kubwa za magharibi na kusini mwa nchi hiyo, ikiwemo mikoa ya Darfur na Kordofan Kusini.
Sudan imeendelea kukabiliwa na mapigano makali kati ya jeshi la nchi hiyo na kikosi cha RSF yaliyoanza mwezi April, 2023, na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine mamilioni wakikosa makazi na kuwa wakimbizi wa ndani na nje ya nchi hiyo, na kuongeza mgogoro mkubwa wa kibinadamu nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma