Tamasha la Filamu la China lafunguliwa nchini Zimbabwe

(CRI Online) Agosti 06, 2025

Tamasha la Filamu la China limefunguliwa jana jumanne katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, ambapo wapenzi wa filamu walikusanyika katika jumba maarufu la filamu la Westgate kusherehekea mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Zimbabwe.

Tamasha hilo lilifunguliwa kwa filamu iliyochezwa na msanii maarufu wa China, Jackie Chan inayoitwa Panda Plan, na kuvutia wageni waalikwa wakiwemo maofisa wa serikali, watengeneza filamu, na wapenzi wa filamu.

Kabla ya tamasha hilo kuanza, Naibu Waziri wa Michezo, Burudani, Sanaa na Utamaduni wa Zimbabwe, Emily Jesaya alisisitiza kuwa nafasi ya tamasha hilo ni kuimarisha uhusiano wa pande mbili kupitia filamu.

Naye Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amezungumza katika tamasha hilo, na kusisitiza nguvu ya filamu inayovuka mipaka na kuongeza maelewano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha