EAC yazindua dhamana ya forodha ili kukuza biashara ya kikanda

(CRI Online) Agosti 06, 2025

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezindua rasmi EACBond ambacho ni chombo cha kiuvumbuzi cha dhamana ya forodha ya kikanda inayolenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

EACBond iliyozinduliwa Jumatatu huko Kampala, mji mkuu wa Uganda, imechukua nafasi ya dhamana tofauti za kitaifa za forodha kwa kutumia mfumo wa pamoja, ikiwasaidia wafanyabiashara kuhakikisha usalama wa usafirishaji wa mizigo yao chini ya dhamana moja.

EAC imesema hatua hiyo inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za biashara, ucheleweshaji katika maeneo ya mpakani, na kufungua mitaji iliyofungwa katika amana za dhamana.

Pia imesema kipindi cha majaribio kitahusisha Uganda, Kenya na Rwanda, na huku mipango ikiendelea kuanza mfumo huo kwa nchi nyingine wanachama wa EAC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha