Rwanda yakubali kupokea wahamiaji 250 chini ya makubaliano mapya na Marekani

(CRI Online) Agosti 06, 2025

Rwanda imefikia makubaliano na Marekani kupokea wahamiaji 250, na kuthibitisha dhamira yake ya muda mrefu ya kusaidia watu waliokimbia makazi yao na kuwasaidia kurejea tena katika jamii.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Bibi Yolande Makolo amesema, karibu kila familia ya Rwanda imepitia wakati mgumu wa kukimbia makazi, na maadili ya kijamii ya Wanyarwanda yamejengwa juu ya maingiliano na kurejeshwa tena katika jamii. Amesema wahamiaji watakaokubaliwa watapewa mafunzo ya kazi, huduma za afya, na msaada wa makazi ili kuwasaidia kuanza maisha yao nchini Rwanda, na kuwapa fursa ya kuchangia moja ya uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika muongo uliopita duniani.

Chini ya makubaliano hayo, Rwanda inabaki na mamlaka ya kukagua na kuidhinisha kila pendekezo la makazi mapya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha