

Lugha Nyingine
Kampuni ya Utengenezaji wa droni DJI yaingia kwenye eneo la usafishaji nyumba kwa kuzindua roboti ya kufanya usafi
![]() |
Mfanyakazi akitambulisha bidhaa kwa mgeni kwenye banda la DJI kwenye Maonesho ya 5 ya Bidhaa za Matumizi Duniani ya China huko Haikou, Hainan, China, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Sun Xiaotian) |
SHENZHEN, Agosti 6 (Xinhua) – Kampuni kubwa ya utengenezaji wa Droni ya China, DJI, imeingia kwenye soko la kidigitali kusafisha nyumba, na kutoa kifaa chake cha kwanza cha kusafisha ndani ya nyumba, na kupanua utaalamu wake wa kiteknolojia zaidi ya kutengeneza droni.
Bidhaa hiyo mpya inayoitwa DJI ROMO, inaunganisha uwezo wa kufagia na kudeki, ikiboresha uwezo wa kampuni wa kutambua hali ya mazingira na teknolojia ya upangaji wa njia iliyoboreshwa hapo awali, kutokana na shughuli zake za droni. Msemaji wa DJI yenye makao yake mjini Shenzhen Zhang Xiaonan amesema, “ROMO inawakilisha mabadiliko ya kwanza ya kimkakati ya DJI kutoka kutengeneza droni hadi vifaa vya kusafisha nyumbani.”
Ingawa sakafu za nyumbani zinatofautiana na mazingira ya angani, kanuni ya msingi ni ile ile yaani kutumia uongozaji njia kwa akili bandia, kutambua mazingira, na kuudhibiti kwa usahihi ili kuwezesha mashine kuhudumia watu kwa ufanisi zaidi.
Utaalam wa kampuni ya DJI unaiwezesha kukabiliana na changamoto muhimu katika utengenezaji wa vifaa vya kufanya usafi. Kampuni hiyo imesema ROMO inatarajiwa kuzinduliwa katika masoko ya ng'ambo baadaye mwaka huu, ingawa tarehe maalum ya uzinduzi na maeneo yatakayopata huduma bado havijathibitishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma