

Lugha Nyingine
Jeshi la anga la Sudan lashambulia ndege ya Emirates iliyobeba askari wa kukodiwa kutoka Columbia
Kituo cha televisheni cha Sudan kimeripoti kuwa, Jeshi la anga la nchi hiyo limeshambulia ndege ya Emirates iliyobeba askari wa kukodiwa kutoka Columbia wakati ilipokuwa inatua katika uwanja wa ndege unaodhibitiwa na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) mkoani Darfur, magharibi mwa Sudan.
Kituo hicho kikinukuu vyanzo vya habari vya jeshi, kimesema jeshi la anga la Sudan lilifanya shambulio la kushtukiza katika njia ya ndege ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyala mkoani Darfur Kusini mapema jana, na lililenga kundi la askari wa kukodiwa kutoka Columbia wakati wakiwasili kwa ndege binafsi inayoaminika kutoka katika moja ya kambi za jeshi za nchi za Ghuba.
Kituo hicho kimesema, askari hao wa kukodiwa waliletwa kukisaidia kikosi cha RSF kama sehemu ya njama za nchi za kigeni zinaolenga kudhoofisha Sudan na kuendeleza vita nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma