

Lugha Nyingine
China na Zimbabwe zasaini makubaliano ya ushirikiano wa msaada wa chakula
Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding na Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi Mthuli Ncube wakipiga picha ya pamoja kwenye hafla ya kusaini makubaliano huko Harare, Zimbabwe, Agosti 6, 2025. (Tafara Mugwara/Xinhua)
China na Zimbabwe jana jumatano zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi na kubadilishana barua kwa ajili ya awamu mpya ya msaada wa chakula ili kuboresha maendeleo ya jamii na uchumi na usalama wa chakula nchini Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alihudhuria hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika Ikulu, ambapo Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi Mthuli Ncube aliishukuru China kwa kuendelea kuunga mkono sekta mbalimbali za kiuchumi nchini Zimbabwe.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amesema, makubaliano hayo ni ushuhuda wa uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili, na kithibitisho cha mshikamano usioyumba wa China kwa Zimbabwe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma