Mawaziri wawili wa Ghana wafariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi

(CRI Online) Agosti 07, 2025

Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Edward Kofi Omane Boamah

Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Februari 26, 2025 ikionesha Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Edward Kofi Omane Boamah. (Seth/Xinhua)

Mnadhimu Mkuu wa Ikulu ya Rais ya Ghana Julius Debrah amesema, watu wanane wakiwemo mawaziri wawili wa nchi hiyo wamefariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi iliyotokea Jumatano karibu na eneo la Adansi katika Mkoa wa Ashanti.

Akizungumza na wanahabari, Debrah amesema miongoni mwa watu waliofariki ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Edward Kofi Omane Boamah na Waziri wa Mazingira, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi Murtala Muhammed, pamoja na wafanyakazi watatu waliokuwa ndege hiyo.

Serikali imeamuru bendera zote za kitaifa zipeperushwe nusu mlingoti hadi taarifa nyingine zitolewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha