China yakamilisha majaribio yake ya kwanza ya kutua kwenye mwezi na kuondoka kwa chombo cha kubeba binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2025
China yakamilisha majaribio yake ya kwanza ya kutua kwenye mwezi na kuondoka kwa chombo cha kubeba binadamu
Picha hii ya kumbukumbu inaonyesha chombo chenye binadamu cha kutua kwenye mwezi kwenye eneo la majaribio la Huailai, Mkoa wa Hebei kaskazini mwa China. (Chanzo cha picha: CNSA)

HUAILAI, Hebei, Agosti 7 (Xinhua) – Jana Alhamisi China ilitangaza kukamilisha kwa mafanikio majaribio ya kina ya chombo chake kutua na kuruka kwenye mwezi katika eneo la majaribio la Huailai, Mkoa wa Hebei kaskazini mwa China. Shirika la Mambo ya Anga ya Juu la China limesema majaribio hayo yaliyokamilishwa Jumatano, ni hatua muhimu katika maendeleo ya mpango wa China wa uchunguzi wa mwezi, na pia ni mara ya kwanza kwa China kufanya majaribio ya uwezo wa kutua na kuruka kwa chombo cha anga ya juu kwenye mwezi.

Chombo hicho kilichopewa jina la Lanyue, ambayo ina maana ya kukumbatia mwezi, ina moduli ya kutua na ya kusonga mbele. Ni chombo kipya kilichoundwa ili kusaidia kazi ya wanasayansi kwenda na kurudi kutoka kwenye mwezi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha